Kilele cha Maadhimisho ya siku ya vijana dunia (12 Agosti) 2025 ambayo kitaifa yamefanyika Dodoma
Kilele cha Maadhimisho ya siku ya vijana dunia (12 Agosti) 2025 ambayo kitaifa yamefanyika Dodoma katika ukumbi wa Mabeyo Complex Hall yakiwa na kauli mbiu “Nguvu Kazi ya Vijana Tanzania kwa Maendeleo Endelevu” na mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiongozana na Naibu katibu Mkuu wa Wizara Bi Zuhura Yunus.
Vijana 100 kutoka mikoa mbalimbali walihudhuria, mashirika ya kimataifa na kitaifa, Asasi za kiraia, viongozi wa serikali, dini, pamoja na wadau wengineo.
KIWOHEDE chini ya Mkurugenzi Mahiri Justa Mwaituka ikiwa ni mojawapo ya shirika liloshiriki kikamilifu kwa kupeleka vijana 100 wanufaika wa mradi unaofadhiliwa na UNFPA, kuweka banda la maonyesho pamoja na tenti la kutolea huduma rafiki kwa vijana kutoka kwa watoa huduma waliobobea kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma.