info@kiwohede.or.tz +255 22 2861 111

KIWOHEDE – Kiota Women’s Health and Development Organization ni shirika lisilokuwa la kiserikali, lililoanzishwa mwaka 1998 na kusajiriwa mwaka 1999. Makao makuu yake ni Dar es Salaam, Buguruni Malapa, wilaya ya Ilala. Na lina matawi Mbeya, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Mtwara, Ruvuma na Iringa pia linafanya kazi kwenye wilaya 23 nchi nzima.

Lengo kuu la shirika Lengo kuu katika Shirika la KIWOHEDE ni kutetea na kulinda afya, haki na maendeleo ya mama na mtoto pamoja kupinga unyanyasaji wa kijinsia na kuwatambua, kuwaondoa na kuwaunganisha watoto walioko katika mazingira magumu na familia zao.

Maono ya shirika:

  • Kuwa na jamii ambapo watoto, vijana na wanawake wapo huru kutoka kwenye aina zote za ukatili na unyanyasaji wa kingono na wanapata nafasi ya sauti zao kusikika katika jamii.
  • Walengwa wetu wakuu ni wasichana walioko katika mazingira magumu wenye umri wa miaka 9 hadi 18.

Malengo ya Mradi:

  • Kuhamasisha haki za afya ya uzazi kwa watoto, rika balehe na vijana kupitia utoaji elimu ya afya ya uzazi kwa kuzingatia jinsia zote.
  • Kuongeza upatikanaji wa huduma za kliniki na zisizo za kliniki za afya ya uzazi na haki kwa watoto,rika balehe na vijana.
  • Kuchangia kutengeneza mazingira ya uhamasishaji na utekelezaji wa sheria na sera mbalimbali zinahamasisha haki ya afya ya uzazi na haki kwa watoto,rika balehe na vijana.